KUINGIZWA KWA ZAO LA KAHAWA

NA KUANZA KWA KILIMO CHAKE KATIKA JAMII YA

WAMERU WA KASKAZINI MWA TANZANIA

Kuingizwa na kuanza kwa kilimo cha kahawa katika jamii ya wa-Rwa au Wameru wanaoishi upande wa Kusini Mashariki mwa miteremko ya Mlima Meru, Kaskazini mwa Tanzania, ambao ni jamii ya wakulima wenye idadi ipatayo 250,000, kunaonyesha waziwazi historia na maendeleo ya kilimo cha biashara barani Afrika.  Kimsingi, kufanikiwa kwa kilimo hicho cha kahawa miongoni mwa Wameru ni matokeo ya sera za Ukoloni ambao ulikuwa umeimarika katika jamii hiyo ambapo Wakoloni walitaka kilimo hicho kiwanufaishe wao zaidi.  Hali hiyo siyo ya kipekee japo ni tofauti na sehemu kubwa ya hali ilivyokuwa katika maeneo mengine ya Afrika ambapo kilimo cha biashara kilikuwa kikiendeshwa na wazawa baada ya kulazimishwa na wakoloni na siyo wakoloni wenyewe waliokiendesha. 

Kuanzia mwaka 1954 na kuendelea, Wameru walikuwa ndio waanzilishi wa mfumo mpya wa kimaendeleo ambapo kupitia kiongozi wao wa kijadi walimleta mtaalamu kutoka Marekani na kumlipa kwa ajili ya kuwasaidia Wameru juu ya kuendeleza kilimo chao cha kahawa. Kufika kwa mtaalamu huyo kulileta mafanikio makubwa, jambo ambalo ni la kujivunia sana ikilinganishwa na ilivyozoeleka kuwa miradi mingi ya maendeleo barani Afrika haifanikiwi.


 


Kahawa.pdf
Document Adobe Acrobat 207.4 KB